KARIBU UWASATA

Umoja wa Wanasalamu Tanzania - Kuimarisha Urithi wa Salamu na Ushirikiano wa Kijamii

KUHUSU SISI

Umoja wa Wanasalamu Tanzania (UWASATA) ni jumuiya ya kitaifa isiyo ya kiserikali inayowaunganisha watuma salamu pamoja na wadau wa mawasiliano, urithi wa kitamaduni na mshikamano wa kijamii.

⏳ Mwanzo

UWASATA ilianzishwa mwaka 2006

📝 Usajili

Ilisajiliwa rasmi kwa REG. NO. 18442 mnamo 29 Oktoba 2012

👥 Uanachama

Wanachama hai zaidi ya 642 na wadau zaidi ya 1,000 kote Tanzania

MADHUMUNI

1 Kujenga Umoja na Udugu

Kujenga umoja na udugu miongoni mwa wanachama na watanzania popote Tanzania

2 Kujikwamua katika Umasikini

Kujikwamua katika umasikini kwa kuunda miradi mbalimbali ya uchumi na kuendeleza vitega uchumi kwa maendeleo ya wanachama watanzania

3 Kushirikiana kwenye Kazi za Umoja

Kushirikiana kwenye kazi zinapotokea za umoja kwa manufaa ya chama

4 Kusaidia na Kuinua Hali ya Jamii

Kusaidia na kuinua hali ya vijana, wanawake, yatima pia kuongeza ari ya vijana kujituma na kuepukana na uvivu

5 Kushirikiana na Mashirika Mengine

Kushirikiana na chama au jamii nyingine yoyote yenye muelekeo na malengo ya umoja huru

MWANACHAMA

VILE VYA KUJIUNGA

  • Tunapokea wanachama wanawake na wanaume
  • Mwanachama lazima afuate na kutekeleza azma na malengo ambayo yameainshwa katika katiba
  • Mwanachama anatakiwa awe na umri usiopungua miaka 18
  • Pia anatakiwa kuwa na akili timamu
  • Kushiriki vipindi mbalimbali vya radio pamoja na kutuma salamu na kusikiliza

JINSI YA KUPATA KATIBA

Kupata katiba na taratibu za kujiunga tafadhali piga simu kwa namba zifuatazo:

+255 0742 588 889
+255 0715 310 413

THAMANI ZETU

Heshima na urithi wa salamu

Tunazikumbati mila na desturi za kisalamu za makundi yote

Mshikamano wa kijamii

Tunajenga mahusiano ya kudumu kati ya wanachama

Upendo na ushirikiano na watu

Tunakuza uhusiano mwema na jamii mbalimbali

Kujenga Jamii yenye maadili mema

Tunaimarisha maadili bora katika jamii zetu

Kujenga umoja kupitia salamu katika Vyombo mbalimbali vya habari

Kupitia radio tunatimiza azma ytu ya kuleta umoja na kusalimiana

SHUGHULI ZETU

Kutuma na Kupokea Salamu kupitia Radio

Kushirikiana na vyombo vya habari kwa kutuma na kupokea salamu kwa jamii yetu pana

Uvuvi na Usindikaji wa Samaki

Kuendeleza uvuvi wa kisasa na usindikaji wa samaki kwa ajili ya chakula na biashara

Ufugaji wa Nyuki

Kufuga nyuki kwa uzalishaji wa asali na bidhaa nyingine za nyuki kwa ajili ya afya na kipato

Upandaji wa Miti (Yambao na Matunda)

Kupanda na kulinda miti ya mbao na miti ya matunda kwa ajili ya mazingira na kipato

Kuandaa Mikutano ya Wanasalamu

Kupanga na kuandaa mikutano ya kila mwezi kwa ajili ya kujadili mambo muhimu na kuimarisha ushirikiano

Kuandaa Semina na Mafundisho ya Ujasiriamali

Kupata nafasi ya kuandaa mafunzo ya ujasiriamali ili kujikwamua kiuchumi

MAWASILIANO

📍 Anwani ya Ofisi

Magomeni Sokoni, Dar es Salaam

📮 Anwani ya Posta

BOX 40911 DAR ES SALAAM

⏰ Muda wa Kazi

Asubuhi mpaka Jioni (03:00 AM - 012:00PM)

📞 Namba za Simu

+255 0742 588 889
+255 0715 310 413

📧 Barua Pepe

info@uwasata.or.tz